Mahakama EAC yakataa pingamizi la mradi wa bomba la mafuta
30 Novemba 2023Mahakama ya kikanda imetupilia mbali pingamizi la kisheria kuhusu mradi wa bomba la mafuta wa mabilioni ya dola nchini Tanzania na Uganda ambao umekosolewa vikali na wanaharakati wa mazingira na wale wa haki za binadamu.
Soma pia:Uganda yatafuta ufadhili wa China kwenye ujenzi wa bomba
Jopo la Majaji watano wa Mahakama ya Afrika Mashariki yenye makao yake jijini Arusha, wametoa uamuzi hapo jana kwamba haikuwa na mamlaka ya kusikiliza pingamizi lililowekwa na mashirika kadhaa ya kiraia kwa sababu liliwasilishwa kuchelewa.
Bomba hilo ni sehemu ya mradi wa dola bilioni 10 unaoongozwa na kampuni kubwa ya nishati ya Ufaransa ya TotalEnergies ambao unalenga kuendeleza vyanzo vya nishati hiyo huko Uganda na kusafirisha mafuta ghafi hadi Tanzania kwa mauzo ya nje.