Mahakama ya Equador yawahukumu waliomuua Villavicencio
13 Julai 2024Mahakama ya Ecuador imemhukumu mwanachama wa genge Carlos Angulo kifungo cha karibu miaka 35 gerezani siku ya Ijumaa kwa kupanga njama na kuamuru mauaji ya mwandishi wa habari aliyegeuka kuwa mgombea wa urais anayepinga ufisadi.
Watu wengine watano pia wamehukumiwa vifungo vikali kwa kuhusika katika mauaji ya Fernando Villavicencio, ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi mwaka jana kabla ya uchaguzi wa nchi hiyo.
Soma zaidi. Makamu wa zamani wa rais wa Equador alazwa hospitalini
Hukumu iliyosomwa mahakamani imearifu kuwa Carlos Angulo, 31, amehukumiwa kifungo cha miaka 34 na miezi minane kwa kupanga na kuamuru mauaji hayo.
Kifo cha Villavicencio kilimhusisha pia rais wa zamani wa nchi hiyo Rafael Correa ambaye yuko uhamishoni nchini Ubelgiji baada ya kukutwa na hatia kwa makosa ya rushwa mwaka 2020. Ingawa mara zote amekanusha shutma hizo.