Mahakama yabatilisha uamuzi wa kusitisha Bunge Ghana
31 Oktoba 2024Hatua hiyo ilisitisha kikamilifu shughuli zote za kisheria chini ya miezi miwili kabla ya uchaguzi mkuu wa nchi hiyo, ambao unatarajiwa kuwa kinyang'anyiro kikali wakati ambapo nchi hiyo inajaribu kujifufua kiuchumi kufuatia mzozo mkubwa wa kifedha.
Hapo jana, Jaji Mkuu Gertrude Torkornoo, alisema kwa kuzingatia madhara yasiyoweza kurekebishwa ambayo yanaweza kuyakumba maeneo ya bunge yalio na maelfu ya raia wa nchi hiyo, ilikuwa muhimu kwa mahakama hiyo kushughulikia mzozo huo mara moja.
Mgogoro huo ulichochewa na msuguano kati ya chama tawala cha Rais Nana Akufo-Addo cha New Patriotic Party (NPP) na chama cha upinzani cha National Democratic Congress (NDC) kilichopata ushindi mdogo baada ya wabunge wanne kujitoa.
Katiba ya Ghana inawazuia wabunge kukihama chama walichochaguliwa chini yake kugombea katika chama kingine au kama wagombea wa kujitegemea.