Mahakama ya Haki Afrika:Tunisia iruhusu wafungwa kuwasiliana
12 Septemba 2023Mahakama imeipa siku 15 serikali ya nchi hiyo ya Afrika ya kaskazini, kuwafahamisha wafungwa, familia, na wanasheria wao, sababu za kuzuiliwa kwao,kulingana na misingi ya kisheria.
Mwezi Mei mwaka huu, wanafamilia wa wafungwa wanne mashuhuri nchini Tunisia na ndugu mmoja wampinzani aliyeuwawa, waliwasilisha shauri katika Mahakama hiyo ya haki za binadamu, wakiitaka iiamuru serikali ya Tunisia kuwaachia huru mara moja wafungwa hao wa kisiasa.
Soma pia:Waziri Mkuu wa Tunisia afutwa kazi katikati mwa matatizo ya kiuchumi
Wafungwa hao wa kisiasa ni pamoja na Rached Ghannouchi, Spika wa bunge na kiongozi wa Chama cha upinzani cha Ennahda, Mbunge na mpinzani mashuhuri wa serikali ya Tunisia, Said Ferjani, Ghazi Chaouachi katibu mkuu wa zamani wa chama cha upinzani cha Tayyarr na Noureddine Bhiri ambaye ni mbunge na waziri wa zamani wa Tunisia.