1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaHong Kong

Mahakama ya Hong Kong yampata na hatia Jimmy Lai

15 Desemba 2025

Mahakama ya Hong Kong imempata na hatia tajiri anayeunga mkono demokrasia Jimmy Lai, kwa kushirikiana na nguvu za kigeni katika mpango wa kuyumbisha usalama wa taifa.

Tajiri wa Hong Kong anayeunga mkono demokrasia Jimmy Lai
Tajiri wa Hong Kong anayeunga mkono demokrasia Jimmy Lai aliyepatwa na hatiaPicha: Henry Nicholls/AFP

Hii ni kesi muhimu zaidi inayohusu sheria tata ya Usalama wa Taifa iliyowekwa na China.  Jimmy Lai  mwenye umri wa miaka 78, anaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kukutwa na hatia ya kuchochea maandamano ya mwaka 2019 ya kudai demokrasia ambayo yalichukuliwa kama changamoto kubwa kwa utawala wa Beijing.

Viongozi wa Ulaya, Marekani na hata mashirika ya kutetea haki za binaadamu wamekosoa hatua hiyo ya Mahakama wakisema imechochewa kisiasa, huku China ikiipongeza Hong Kong kwa kuadhibu kile ilichotaja kuwa "vitendo vya uhalifu vinavyohatarisha usalama wa taifa".

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW