Mahakama ya ICC yaionya Jubilee, Kenya
4 Septemba 2013Mahakama ya kimataifa inayoshughulikia kesi za uhalifu, ICC, ya mjini The Hague Uholanzi imeuonya muungano wa Jubilee kwa nia yake ya kutaka kuiondoa Kenya kutoka kwa mkataba wa Roma ulioiunda mahakama hiyo. Mahakama hiyo imesema hatua hiyo haitasaidia kuzikwamisha kesi zinazowakabili viongozi wa muungano huo. Kesi dhidi ya Makamu wa rais, William Ruto, pamoja na mwanahabari Joshua Arap Sang, inatarajiwa kuanza katika mahakama hiyo Septemba 10 huku rais Uhuru Kenyatta akitarajiwa kwenda Hague Novemba 12 mwaka huu kwa ajili ya kujibu mashitaka kuhusiana na machafuko ya baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 nchini Kenya.
Sikiliza mahojiano kati ya Josephat Charo na mwanaharakati wa haki za binaadamu na haki za kiraia nchini Kenya, Gachihi Gacheke, ambaye kwanza anatoa maoni yake kuhusu mambo yanavyokwenda katika kesi za viongozi hao wa Jubilee. Kusikiliza mahojiano haya tafadhali bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.
Mwandishi: Josephat Charo
Mhariri: Yusuf Saumu