Mahakama ya ICC yatimiza miaka 20
17 Julai 2018Hii ni mahakama inayotekeleza sheria za kimataifa na kuwaadhibu wahalifu , bila kujali wanatokea wapi. Hilo ndio lilikuwa wazo la msingi la kuundwa kwa mahakama hii ya kimataifa ya ICC.
Kilikuwa ni kikao kilichokuwa na mvutano , Julai 1998 mjini Rome. Ilichukua miaka mitatu ya malumbano makali katika Umoja wa mataifa kuweza kuunda mahakama hii ya kimataifa ya uhalifu ICC mjini The Hague. Kikao cha siku tatu cha kamati maalum ya baraza kuu la Umoja wa mataifa kilichoketi kwa muda wa siku tatu kilifanikisha kupitishwa kwa azimio la baraza kuu , kuhusiana na mkataba wa kuundwa mahakama hiyo ya kimataifa.
Zilikuwa juhudu maalum za waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani wa wakati huo Klaus Kinkel zilizofanikisha kuundwa kwa mahakama hiyo huru ya uhalifu. Ilikuwa kutoka mahakama ya Umoja wa mataifa ya uhalifu wa kivita kwa ajili ya iliyokuwa Yugoslavia ya zamani na mahakama ya Umoja wa mataifa ya mauaji ya kimbari nchini Rwanda, ambapo mahakama hizo mbili ziliwekwa pamoja na kuunda mahakama ya ICC.
Baraza la Usalama
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa iliifanya mahakama hiyo mwanzoni mwa miaka ya 90 kuwa chini yake.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliteua majaji na waendesha mashitaka na kuwa na ushawishi hadi wakati huo wa uwezekano wa kuifunga mahakama hii wakati wowote. Kwa kuwa ilitaka aina nyingine ya mahakama kama hiyo.
Baraza la Usalama lilitaka kuweka azimio la kuichunguza mahakama hiyo na kuidhibiti. Lakini kutokana na kushindwa kwa mataifa kutimiza masharti ya kuingia katika mahakama hiyo, baadhi ya mataifa yalizuiwa kuingia katika mahakama hiyo. Mfano ni Libya na Sudan.
Kutokana na utata wa kisheria , ambao ni sheria ya kutowajibika kisheria, Marekani ilikataa kujiunga na mahakama hiyo. Na iwapo ingejiunga basi wanajeshi wa Marekani kutokana na kuhusika duniani kote kijeshi wangefikishwa katika mahakama hiyo. Pia Marekani ilikataa suala la uchokozi, ambalo lilikuwa ni kosa kuishambulia nchi nyingine.
Mwandishi: Sabine Kinkartz / ZR / Sekione Kitojo
Mhariri:Josephat Charo