SiasaUholanzi
ICJ kuamua juu ya mamlaka ya kusikiliza kesi dhidi ya Urusi
2 Februari 2024Matangazo
Mahakama ya ICJ ambayo ni mahakama ya juu kabisa ya Umoja wa Mataifa itaamua iwapo inaruhusiwa kusikiliza shauri hilo.
Ukraine ilimshitaki jirani yake Urusi muda mfupi baada ya uvamizi kamili mwaka 2022, ikiishutumu Moscow kwa kukiuka mkataba unaopinga mauaji ya kimbari.
Urusi inakana madai hayo na imeomba kesi hiyo kutupiliwa mbali.
Ukraine kwa upande wake inaungwa mkono katika madai yake mbele ya mahakama ya ICJ na washirika wake wa nchi 32 za Magharibi.
Awali, Urusi ilikuwa imetetea uvamizi wake nchini Ukraine kwa kusema kwamba mauaji ya halaiki ya Warusi nchini Ukraine yalipaswa kuzuiwa.