Mahakama ya ICJ yaiagiza Syria kukomesha mpango wa mateso
17 Novemba 2023Mahakama hiyo imesema kuwa lazima Syria ichukue hatua zote zilizo ndani ya uwezo wake ili kuzuia vitendo vya mateso na vitendo vingine vya kikatili, vya kinyama au vya kudhalilisha au adhabu. Mahakama hiyo pia imeamua kuwa lazima Syria izuie uharibifu na kuhakikisha uhifadhi wa ushahidi wowote unaohusiana na mateso.
Canada na Uholanzi zatoa taarifa ya pamoja kuhusu Syria
Katika taarifa ya pamoja, serikali za Canada na Uholanzi, zimesema kuwa mahakama hiyo imetambua udharura wa hali hiyo na madhara yasiyoweza kurekebishwa yanayosababishwa na mateso ya mara kwa mara na dhuluma nyingine za Syria dhidi ya watu wake.
Uamuzi huo unakuja baada ya Ufaransa kutoa waranti ya kimataifa ya kukamatwa kwa Rais wa Syria Bashar al-Assad, anayetuhumiwa kuhusika na uhalifu dhidi ya binadamu kutokana na mashambulizi ya kemikali ya mwaka 2013.