1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

ICJ yaiunga mkono Guinea ya Ikweta katika mzozo na Gabon

Josephat Charo
20 Mei 2025

Mahakama ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia masuala ya haki ICJ siku ya Jumatatu iliiunga mkono Guinea ya Ikweta katika mzozo wa miongo kadhaa kati yake na Gabon kuhusu visiwa.

Guinea ya Ikweta na Gabon ziliiomba mahakama ya ICJ kutafuta suluhisho la amani kuhusu mzozo wa visiwa.
Guinea ya Ikweta na Gabon ziliiomba mahakama ya ICJ kutafuta suluhisho la amani kuhusu mzozo wa visiwa.Picha: Valerio Rosati/Zoonar/picture alliance

Mataifa mawili ya Afrika Magharibi, Guinea ya Ikweta na Gabon, yamekuwa yakizozania kisiwa cha Mbanie chenye ukubwa wa hekta 30 na visiwa viwili vidogo vya ukanda wa chini, Cocotiers na Conga, tangu mwanzoni mwa miaka ya 1970.

Visiwa hivyo ni vidogo na havikaliki lakini viko katika eneo ambalo linaweza kuwa na mafuta na gesi nyingi.

Mzozo huo ulianza mwaka wa 1900, wakati mamlaka ya kikoloni Ufaransa na Uhispania zilipoitia saini mkataba huko Paris kuweka mipaka kati ya nchi hizo mbili. Lakini Gabon ilisema kuwa mkataba wa baadaye, Mkataba wa Bata wa 1974, ullisawazisha mpaka wa visiwa hivyo kwa niaba yao. 

Hata hivyo, Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ iliamua kwamba Mkataba wa Bata "ulioitishwa na Jamhuri ya Gabon sio mkataba wenye nguvu ya sheria na haujumuishi hati ya kisheria ya umiliki.

Ilisema kwamba hatimiliki ya kisheria ya visiwa hivyo ilikuwa inashikiliwa na Uhispania, ambayo baadaye ilipitishwa kwa Guinea ya Ikweta baada ya kupata uhuru mnamo 1968.

Mahakama ya ICJ yatupilia mbali kesi ya Sudan

Tofauti na mataifa mengi yaliyofikishwa mbele ya mahakama ya ICJ mjini The Hague, ambayo hupitisha hukumu katika mizozo kati ya mataifa, Guinea na Guinea ya Ikweta zilikubaliana kuwaomba majaji watoe uamuzi katika juhudi za kutafuta suluhu la kirafiki.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW