Sheria na HakiKenya
Mahakama ya Juu Kenya yaidhinisha sheria ya fedha, 2023
8 Septemba 2023Matangazo
Sheria hiyo inalenga kuongeza maradufu kodi ya ongezeko la thamani kwenye bidhaa za mafuta. Aidha inaongeza tozo mpya iliyoanzishwa kwa ajili ya kuwezesha ujenzi wa nyumba.
Sheria hiyo iliyoanza kutekelezwa Julai 28 , ilisababisha ghadhabu zilizofuatiwa na maandamano ya kupinga ugumu wa maisha nchini Kenya katika mwezi huo wa Julai.
Serikali ya Rais William Ruto imesema kodi za juu ni muhimu katika kusaidia kukabili ongezeko la deni na kufadhili mipango ya kubuni nafasi za ajira.