Mahakama ya Juu Nigeria yabatilisha muundo wa sarafu mpya
4 Machi 2023Matangazo
Oktoba mwaka uliopita, serikali ilitangaza mpango wa kutengeneza noti mpya na ikawapa raia wake muda wa hadi mwishoni mwa mwezi Januari kubadilisha sarafu yao ya zamani.
Hata hivyo, Jaji Emmanuel Agim alisema taratibu zinazofaa hazikufuatwa na noti chache mpya ndiyo zilitolewa.
Soma zaidi: Nigeria yaweka kikomo cha utoaji pesa zilizopo benki
Benki Kuu ilisema utengenezaji wa sarafu mpya ungeathiri mfumuko wa bei, lakini majimbo 16 yaliupinga mpango huo mahakamani, yakisema hayakupewa muda wa kutosha kufanya mabadiliko.
Mahakama ya Juu iliamua kwamba noti za zamani zinapaswa kuzingatiwa katika zabuni halali hadi ifikapo mwishoni mwa mwaka 2023.