1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiAsia

Mahakama ya juu Pakistan yakubali kumuachia Imran Khan

22 Novemba 2023

Mahakama ya Juu ya Pakistan leo imekubali ombi la dhamana la waziri mkuu wa zamani Imran Khan. Haya ni kwa mujibu wa wakili wake.

Pakistan | Waziri Mkuu wa zamani Imran Khan
Sheria na haki | Waziri Mkuu wa zamani Pakistan Imran KhanPicha: Akhtar Soomro/REUTERS

Uamuzi huu wa mahakama hiyo unakuja siku moja baada ya mahakama nyengine kutangaza kuwa kinyume cha sheria kesi nyingine inayomkabili ya kuvujisha siri za serikali.

Khan ambaye ni nyota wa zamani wa mchezo wa kriketi, anakabiliwa na mashtaka kadhaa mahakamani akiwa na matumaini ya kuachiwa na kukiongoza chama chake katika kampeni ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Februari 8, ambapo hasimu wake, waziri mkuu mwengine wa zamani anatumai kushinda.

Soma pia:Mahakama Pakistan yamfungulia kesi nyingine Imran Khan

Khan mwenye umri wa miaka 71 alifungwa kwa miaka mitatu jela mnamo Agosti 5 kwa kuuza zawadi za serikali wakati wa utawala wake kati ya mwaka 2018 na 2022.

Aliondolewa madarakani mwaka 2022 baada ya kupoteza kura ya kutokuwa na imani naye bungeni. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW