Mchakato wa kusikiza hoja kuhusu wahamiaji kuanza Uingereza
9 Oktoba 2023Mchakato huo unaanza baada ya serikali ya chama cha Conservative kukataa rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama ya rufaa wa mwezi Juni, ambao ulisema mpango huo wa serikali ni kinyume cha sheria, kwa sababu Rwanda sio nchi salama.
Marekani na nchi za Ulaya zapambana na mawimbi ya wahamiaji
Haya yanajiri wakati Marekani na nchi nyingi za Ulaya zikipambana kutafuta njia bora ya kukabiliana na mawimbi ya wahamiaji wanaoingia katika nchi hizo kutafuta hifadhi, wakikimbia vita, ghasia na ukandamizaji, pamoja na madhila yanayosababishwa na mabadiliko ya tabianchi.
Soma pia: Brussels yakosa muafaka mgogoro wa wakimbizi
Waziri Mkuu wa Uingereza Rishi Sunak anaupigia upatu mpango huo wa kuwapeleka wahamiaji nchini Rwanda kama suluhisho mwafaka, lakini unapingwa vikali na watetezi wa haki za binadamu pamoja na watu wengi maarufu nchini Uingereza.