Mahakama ya Katiba ya Croatia yamzuwia rais kuwa waziri mkuu
19 Aprili 2024Matangazo
Hatua hiyo inazima azma ya kiongozi huyo ya kutaka kuongoza serikali yoyote ya muungano nchini humo.
Mahakama hiyo ilisema siku ya Ijumaa (Aprili 19) kwamba Rais Milanovic alishindwa kuzingatia onyo lililotolewa mnamo mwezi Marchi la kumtaka kwanza ajiuzulu nafasi ya urais kabla ya kuanza kampeni ya kutaka wadhifa wa uwaziri mkuu.
Soma zaidi: EU yapongeza mafanikio makubwa ya Croatia
Kiongozi huyo wa Croatia mara kadhaa ameukosoa Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Kujihami ya NATO na amekuwa akipinga hatua ya kuisadia Ukraine katika vita vyake na Urusi.