1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama ya kijeshi Uganda yawatia hatiani wapinzani 16

22 Oktoba 2024

Mahakama ya kijeshi nchini Uganda imewatia hatiani hapo jana wanachama 16 wa chama cha upinzani kwa kosa la uhaini na umiliki wa vilipuzi kinyume cha sheria.

Uganda Kampala 2024 | Vikosi vya usalama vinalinda makao makuu ya chama cha kiongozi wa upinzani Bobi Wine
Vikosi vya usalama vya Uganda vikiwa na ulinzi nje ya ofisi za chama cha siasa cha National Unity Platform (NUP) kinachoongozwa na Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, Kampala, Uganda Julai 22, 2024.Picha: Abubaker Lubowa/REUTERS

Upande wa mashtaka umedai kuwa wanachama 16 wa Jukwaa la Umoja wa Kitaifa, pamoja na wengine ambao bado hawajakamatwa, walikutwa na vilipuzi kati ya Novemba mwaka 2020 na Mei 2021, wakati uchaguzi ulikuwa ukiendelea. Kwa mujibu wakili wa upande wa utetezi Shamim Malende amesema kesi hiyo ilikuwa na mashaka kwa jinsi ilivyosikilizwa ambapo baadaye watuhumiwa walikubali makosa ambayo awali waliyakana. Mwimbaji wa zamani na kiongozi wa upinzani Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine, amedai kuwa watu hao wamelazimishwa kukiri makosa yao na kuomba msamaha wa rais. Waandishi wa habari hata hivyo hawakuruhusiwa kuhudhuria kikao hicho. Vijana hao 16 wamekaa gerezani kwa miaka minne, na watafikishwa mahakamani hapo kesho ili kusomewa rasmi hukumu yao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW