1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaKorea Kusini

Mahakama ya Korea Kusini yakataa Rais Yoon kuachiwa huru

16 Januari 2025

Mawakili wa Rais aliyeachishwa kazi na bunge nchini Korea Kusini Yoon Suk Yeol wameshindwa katika juhudi yao ya kuitaka mahakama imuachilie huru.

Korea Kusini | Korea Kusini yamkamata rais wa zamani Yoon Suk Yeol
Wanasheria wa Yoon waliitaka Mahakama ya Wilaya ya Kati ya Seoul kumuachia huru, wakihoji uhalali wa hati ya kuzuiliwa kwake.Picha: Daniel Ceng/Andalou/picture alliance

Hayo yamejiri siku moja tu baada ya Rais Yoon kukamatwa katika makazi yake ili kuhojiwa kuhusu madai ya uasi yanayohusishwa na tamko lake la sheria ya kijeshi mwezi uliopita.

Yoon alipelekwa kizuizini karibu na mji mkuu wa nchi hiyo Seoul, baada ya kuhojiwa kwa zaidi ya saa 10 jana Jumatano katika makao makuu ya Ofisi ya Upelelezi wa Ufisadi kwa Maafisa wa Vyeo vya Juu, ambapo alitumia haki yake ya kukaa kimya.

Yoon amekataa kuhojiwa zaidi leo na maafisa wa kupambana na rushwa huku mawakili wake wakisisitiza kuwa uchunguzi huo ni kinyume cha sheria.

Wanasheria wake waliitaka Mahakama ya Wilaya ya Kati ya Seoul kumuachia huru, wakihoji uhalali wa hati ya kuzuiliwa Yoon iliyotolewa na Mahakama ya Wilaya ya Magharibi ya Seoul. Lakini Mahakama ya Wilaya ya Kati ya Seoul imekataa ombi lao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW