1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPakistan

Mahakama ya Pakistan yazuia Khan kukamatwa

17 Machi 2023

Mahakama kuu ya Pakistan imeufuta waranti wa kumkamata aliyekuwa waziri mkuu Imran Khan, hatua iliyoondoa mkwamo mkali kati ya wafuasi wake na vikosi vya usalama.

Pakistan Lahore | Unterstützer von Ex-Premierminister Imran Khan blockieren Straße um Verhaftung zu verhindern
Picha: Aamir Qureshi/FP

Hatua hiyo ya kumakamata Khan mapema wiki hii iligeuka ghasia wakati wafuasi wake walipopambana na vikosi vya usalama. Vyombo vya habari nchini humo vimesema mahakama kuu ya Islamabad imeifuta amri hiyo ili kumruhusu Khan kufika mahakamani kesho kuhusiana na mashitaka kuwa aliuza kinyume cha sheria zawadi za serikali alizopewa na viongozi wa kigeni wakati akiwa waziri mkuu kuanzia mwaka wa 2018 hadi 2022. Khan anakanusha mashitaka hayo. Tume ya uchaguzi ya Pakistan ilimkuta na hatia na kumzuia kushika wadhifa wa kiserikali kwa muhula mmoja wa bunge.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW