1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaNigeria

Mahakama ya rufaa Nigeria kuamua rufaa ya uchaguzi wa Tinubu

26 Oktoba 2023

Mahakama ya Juu ya Nigeria leo inatarajiwa kutoa uamuzi kuhusiana na ushindi wa Rais Bola Ahmed Tinubu katika kesi ya mwisho ya rufaa iliyowasilishwa na upinzani.

Nigeria gewinnt den Antrag auf Aufhebung des Schadensersatzes in Höhe von 11 Milliarden US-Dollar für den gescheiterten Gasvertrag
Picha: Temilade Adelaja/REUTERS

Kikao cha majaji saba kitatoa uamuzi baada ya mahakama ya chini kutupilia mbali madai ya upinzani ya ukiukaji wa sheria za uchaguzi na Tinubu kutotimiza vigezo vya kuwania urais.

Baada ya uchaguzi wa mwezi Februari, Tume Huru ya Uchaguzi ya Nigeria INEC ilikiri kwamba kulikuwa na matatizo ya hapa na pale katika zoezi la upigaji kura ila ikakanusha madai kwamba uchaguzi haukuwa huru na haki.

Tinubu ambaye alikuwa gavana wa zamani wa Lagos, alipata ushindi wa asilimia 37 dhidi ya wagombea, Atiku Abubakar wa chama cha Peoples demcoratic Party PDP na Peter Obi wa chama cha Labour.