1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaThailand

Mahakama ya Thailand yamuondoa Waziri Mkuu madarakani

15 Agosti 2024

Mahakama ya Thailand imemuondoa madarakani Waziri Mkuu Srettha Thavisin kwa madai ya kukiuka maadili hatua inayozidi kuzitikisa siasa za taifa hilo.

Thailand | Waziri Mkuu Srettha Thavisin
Waziri Mkuu wa Thailand Srettha Thavisin ameondolwa madarakani kwa maamuzi ya mahakama kufuatia shutuma za kukosa uadilifuPicha: Sakchai Lalit/AP Photo/picture alliance

Wiki iliyopita mahakama hiyo iliagiza chama kikuu cha upinzani kuvunjwa.

Mahakama ya Katiba ilitoa uamuzi huo kufuatia madai dhidi ya Srettha ya kumteua waziri aliyefungwa jela kwa tuhuma za kutaka kumhonga afisa wa mahakama. 

Mahakama hiyo ilipiga kura 5 dhidi ya 4 na kuagiza Srettha kuondoka madarakani mara moja.

Baraza la Mawaziri litaendelea na shughuli zake chini ya serikali ya mpito hadi Bunge litakapomuidhinisha Waziri Mkuu mpya.

Kura ya Bunge ilipangwa kufanyika siku ya Ijumaa lakini hakuna ukomo wa wa muda wa kujaza nafasi hiyo. 

Srettha amesema muda mfupi baada ya hukumu hiyo kwamba anaheshimu maamuzi na kwamba alipenda kuheshimu maadili wakati wote wa uongozi wake.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW