1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JamiiUganda

Mahakama ya Uganda yamfungulia Waziri mashtaka ya ufisadi

7 Aprili 2023

Mahakama nchini Uganda imemfungulia rasmi mashtaka ya ufisadi na rushwa Waziri Marie Goretti Kitutu kufuatia tuhma za kuuza mabati 14,500 ya kuezekea nyumba yaliyokusudiwa kuwasaidia raia wa huko Karamoja.

DW Videostill | Tackling food insecurity in Karamoja
Picha: Emmanuel Lubega/DW

Licha ya Waziri Kitutu kukana mashtaka hayo, alirejeshwa rumande na kesi yake itasikilizwa tena ifikapo Aprili 12 mwaka huu. Akihojiwa na Kamati ya Bunge mwezi uliopita, Marie Goretti Gitutu aliomba msamaha kwa usimamizi mbaya wa usambazaji wa mabati hayo.

Mawaziri kushtakiwa kwa ufisadi ni jambo la nadra nchini Uganda, ambako ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za umma ni jambo lililozoeleka.

Karamoja  ni eneo la Uganda linalopakana na mataifa ya Kenya na Sudan Kusini, na wakaazi wake ni wafugaji wanaohamahama ambao wako katika hatari ya kukumbwa na ukame na wizi wa mifugo.