1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Sheria na HakiUrusi

Mahakama ya Urusi yawahukumu vifungo maafisa wa ICC

12 Desemba 2025

Mahakama nchini Urusi imewahukumu kifungo cha muda mrefu gerezani baadhi ya wawakilishi wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC, bila ya watuhumiwa kuwepo mahakamani.

The Hague, Uholanzi | Mahakama ya ICC | Mahakama ya Kimataifa ya Jinai | Kesi ya Mahamat Said Abdel Kani | Mwendesha Mashtaka Mkuu Karim Khan
Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC Karim Khan, katikati, akiingia katika chumba cha mahakama kwa ajili ya kesi ya Mahamat Said Abdel Kani katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai huko The Hague, Uholanzi, Jumatatu, Septemba 26, 2022.Picha: Peter Dejong/AP Photo/picture alliance

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC Karim Khan amehukumiwa kifungo cha miaka 15 gerezani, ambapo miaka tisa ataitumikia gerezani na iliyosalia mahali wanapoadhibiwa wahalifu wakubwa, hii ikiwa ni kulingana na Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Urusi hii leo.

Majaji wanane wa ICC iliyoko mjini The Hague pia wamehukumiwa vifungo vya kati ya miaka mitatu na nusu hadi 15 jela.

Kulingana na Urusi, Khan alifungua kesi haramu za uhalifu dhidi ya raia wa taifa hilo kuanzia mwezi Februari hadi Machi, 2022 na kupelekea kutolewa kwa waranti usio halali wa kumkamata Rais Vladimir Putin, miongoni mwa viongozi wengine.

Hata hivyo, hukumu hiyo haitakuwa na matokeo kwa sasa kwa kuwa Khan hayuko Urusi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW