Mahakama ya Uturuki yatoa waranti wa kukamtwa kwa Netanyahu
8 Novemba 2025
Matangazo
Ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu wa Istanbul ilihalalisha hati hizo na kusema kwamba maafisa wa serikali ya Israeli wanapaswa kuwajibishwa kwa vitendo vya uhalifu dhidi ya ubinadamu na mauaji ya halaiki yaliyofanywa Gaza, pamoja na vitendo vilivyofanywa dhidi ya msafara wa kupeleka misaada katika Ukanda wa Gaza.
Waendesha mashitaka wamesema kuwa, kutokana na uhalifu huo, maelfu ya watu, wakiwemo wanawake na watoto, walipoteza maisha, huku maelfu zaidi wakijeruhiwa na maeneo ya makazi yakiharibiwa.
Mara kwa mara,Israel imeshutumiwa kwa uhalifu wa kivita na, katika baadhi ya matukio, mauaji ya halaiki juu ya matendo yake katika Ukanda wa Gaza, shutuma ambazo imekanusha.