Mahakama yaahirisha mara ya saba kesi ya mwandishi habari
7 Novemba 2019Erick Kabendera, mwandishi habari mwenye makao yake mjini Dar es Salaam ambaye amekuwa akiripoti katika majarida ya kimataifa, ameshitakiwa mwezi Agosti kwa uhalifu wa kupangilia, kukwepa kulipa kodi na utakatishaji fedha.
Jaji katika mahakama ya Kisutu mjini Dar es Salaam ameahirisha kesi hiyo hadi Novemba 20.
Kama kesi nyingine tangu mwezi Agosti, mwendesha mashitaka ameiambia mahakama kuwa uchunguzi bado haujakamilika, wakati mawakili wa Kabendera wametaka kesi hiyo iendelee kutokana na hoja kwamba mteja wao anashikiliwa kwa mashitaka ambayo hayana dhamana.
Jaji anayeshughulikia kesi hiyo amepandishwa cheo kwenda katika mahakama nyingine na jaji mpya hajakabidhiwa kesi hiyo. Mawakili wake na kundi la wanaharakati wa haki za binadamu wanadai kesi hiyo inashawishiwa kisiasa.