1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaPeru

Mahakama yaamuru kuachiliwa huru kwa Fujimori

6 Desemba 2023

Mahakama ya katiba ya Peru imeagiza kuachiliwa mara moja kwa rais wa zamani aliyefungwa jela, Alberto Fujimori.

Rais wa zamani wa Peru, Alberto Fujimori.
Rais wa zamani wa Peru, Alberto Fujimori.Picha: Martin Mejia/AP/picture alliance

Hayo ni kulingana na hati ya mahakama iliyochapishwa Jumanne (Disemba 5) na kuashiria kubadilika kwa kesi hiyo ya kiongozi huyo wa zamani mwenye utata.

Fujimori mwenye umri wa miaka 85, anatumikia kifungo cha miaka 25 kwa ukiukwaji wa haki za binadamu na ufisadi wakati wa utawala wake wa muongo mmoja katika miaka ya 90.

Mahakama ya juu zaidi nchini humo iliamua kwamba rufaa ya kurejeshwa kwa msamaha wa mwaka 2017 kwa Fujimori anayeugua kwa misingi ya kibinadamu, ulikuwa uamuzi sahihi.

Wakili wa Fujimori, Elio Riera, alisema Fujimori huenda angeachiwa siku ya Jumatano (Disemba 6).