Hichilema ana kesi ya kujibu kwa uhaini
26 Aprili 2017Kiongozi huyo wa chama cha United Party for National Development (UPND) alikamatwa katika msako wa polisi nyumbani kwake mwezi huu na alifunguliwa mashitaka ya kujaribu kuipindua serikali katika mahakama kuu. Mawakili wa Hichilema wamekata rufaa, wakisema madai hayo hayaeleweki.
Lakini jaji Greenwell Malumani aliiambia mahakama iliyokuwa imejaa watu kwamba mahakama hiyo haina mamlaka ya kufuta madai hayo na kuipeleka kesi hiyo katika mahakama kuu.
Zambia ilikuwa moja kati ya nchi zenye utulivu mkubwa katika eneo la kusini mwa Afrika hadi pale mahusiano yalipoharibika kati ya serikali na upinzani mwezi Agosti, wakati chama cha Rais Edgar Lungu cha Patriotic Front kukishinda chama cha UPND katika uchaguzi uliogubikwa na machafuko.