1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama yasitisha mgomo wa marubani Lufthansa

Admin.WagnerD9 Septemba 2015

Mahakama ya kazi ya Ujerumani imewaamuru marubani wa shirika la Lufthansa kusitisha mgomo wao ulioanza Jumanne, na kurejea kazini mara moja, ikisema mgomo huo umepoteza lengo.

Deutschland Angehörige auf dem Weg zur Absturzstelle Germanwings A320
Picha: AFP/Getty Images/P. Stollarz

Chama cha umoja wa marubani cha Vereingung Cockpit kimesema uamuzi huo wa mahakama ya kazi ya jimbo la Hessen, unamaanisha kuwa marubani wote laazima warudi kazini mara moja, ingawa haikubainika mara moja ni lini safari za ndege za kampuni hiyo zitarejea kawaida.

Mara nyingi inapotokea migomo, kampuni za ndege huchukuwa muda wa ziada kuweza kuzirejsha ndege mahala pake ili kuanza kutoa huduma kama kawaida.

Chama cha umoja wa marubani kilianzsha mfululizo w migomo karibu miezi 18 iliyopita, ambayo malengo yake ya awali yalikuwa kuzuwia mabadiliko katika mafao ya kustafu mapema, lakini katika miezi ya karibuni, marubani hao wametaka kuzuwia mipango ya Lufthansa kuanzisha shirika tanzu la ndege za gharama nafuu.

Chama cha Vereingung Cockpit kilisema mahakama hiyo ya kazi ya kanda iliyofuta hukumu ya mahakama ya chini iliyoruhusu mgomo huo siku ya Jumanne, iliamua kuwa sababu ya awali ya mgomo, ambayo ni mafao ya kustafu, imewekwa pembeni, na kwamba kiukweli marubani hao wanagoma kwa sababu tofauti.

Ndege za shirika la Lufthanza zikiwa katika uwanja wa ndege wa Frankurt am Main katika kimbo la Hessen.Picha: picture-alliance/dpa/Schmidt

"Tumeshangazwa sana na uamuzi huo. Tutaupitia kwa kina na kisha tujuwe madhara ya kuendelea na mapambano yetu", amesema Markus Wahl, msemaji wa chama cha umoja wa marubani, kufuatia uamuzi wa mahakama.

Uongozi wa Lufthansa uliyokaribisha uamuzi huo wa mahakama, umesema laazima ufaniskishe mpango wa kupunguza gharama ili kuweza kushindana vyema na mashirika ya gharama nafuu kama vile Ryanair, ambalo sasa linalenga kuingia soko la Ujerumani.

Chama cha waajiri cha Ujerumani BDA, kilisema awali kuwa migomo isiyokwisha inaharibu uchumi mzima wa Ujerumani, na kuhoji uhalali wa malengo ya marubani hao wanaogoma. Kufuatia uamuzi wa mahakama leo, hisa za Lufthansa zimepanda kutoka euro 11.62 hadi euro 11.66.

Mgomo huo ulisababisha kufutwa kwa karibu safari 1000 kati ya 1,520 zilizopangwa kufanyika siku ya Jumatano, lilisema shirika hilo kubwa kabisaa la ndege barani Ulaya, na kuongeza kuwa kati ya abiria 180,000 waliokata tiketi za kusafiri siku hiyo ya Jumatano, abiria 140,000 walikosa safari zao.

Mwandishi: Iddi Ssessanga/dpae,rtre,afpe
Mhariri: Mohammed Khelef