1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahakama za kimataifa kuchunguza kuvamiwa Ukraine

Admin.WagnerD7 Machi 2022

Mahakama mbili za kimataifa zimeanza uchunguzi kuhusu vita vya Urusi dhidi ya Ukraine. Kesi moja itaanza Jumatatu hii, nyingine inaweza kumlenga moja kwa moja Rais Putin mwenyewe.

Niederlande Den Haag | Europäischer Gerichtshof
Picha: Yves Herman/REUTERS

Jumatatu hii, Ukraine itapata nafasi katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki ya huko mjini The Hague Uholanzi. Mahakama ya Umoja wa Mataifa, ambayo ina jukumu la kusuluhisha mizozo kati ya nchi mbili, inazingatia zuio ambalo Ukraine imelitoa dhidi ya Urusi chini ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa dhidi mauwaji ya halaiki.

Mwendesha Mashtaka Mkuu wa ICC, Karim KhanPicha: International Criminal Court/dpa/picture alliance

Kimsingi serikali ya Kyiv anawataka majaji wa Umoja wa Mataifa kuainisha shambulio la Urusi kama mauaji ya halaiki na wakati huohuo kuyakanusha madai ya Moscow kwamba Ukraine ilikuwa ikifanya mauaji ya watu wengi dhidi ya Warusi walio wachache huko mashariki mwa nchi hiyo.

Lakini kesho, Jumanne mawakili wa Ikulu ya Urusi, Kremlin wanatarajiwa kukanusha vikali kesi hiyo, huku Urusi yenyewe kama taifa ikiyakata mamlaka ya kisheria ya mahakama hiyo ya mjini The Hague. Serikali ya Moscow itatoa hoja inayosema kwamba hakuna mauaji ya halaiki yanayofanywa na Urusi, hakuna kesi na kwa hivyo hakuna mahakama ambayo inaweza kuwa na mamlaka ya kusimamia haki.

Ugumu wa kupatikana haki

Profesa Kai Ambos, mtaalamu wa sheria za uhalifu za kimataifa kutoka mjini Göttingen, Ujerumani aliiambia DW kwamba, kwa ujumla Urusi na Marekani hazijawahi kuitambua mahakama ya Umoja wa Mataifa lakini badale yake wanaweza kufanya hivyo kwa kutegemea tu, msingi wa kesi. Kwa hivyo profesa huyo, aliongeza kwa kuonesha hali ya kutokuwa na matokeo yeyote ya wazi katika mashtaka hayo ya juma hili kwa Ukraine, ingawa kesi hiyo inavuta hisia za wengi na jinsi zitakavyoshughulika na vita vya Rais Putin.

Lakini pia kuna kesi ya pili inayoendelea hivi sasa katika mahakama nyingine ya kimataifa. Katika kesi hii mwendesha mashtaka tayari ameanza uchunguzi wa iwapo Rais wa Urusi au viongozi wengine wakuu katika serikali yake wanahusika na uhalifu wa kivita au uhalifu dhidi ya ubinadamu nchini Ukraine.

Kwa zingatio la kesi hiyo, akiwa The Hague juma lililopta mwendesha mashtaka mkuu wa hiyo, Karim Khan amenukulikuwa akisema "Nimeridhika kwamba kuna msingi wa kuamini kwamba madai yote mawili ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu yamefanywa nchini Ukraine," Alitoa maagizo kwa waandisha mashtaka wake kuchunguza vitendo hivyo na kupata ushahidi na timu ya kwanza ipo Ukraine.

Hoja inasalia kuwa kuna uwezekano wa Rais Putin siku moja akapandishwa kizimbani kama kesi hiyo itaendelea, Profesa Kai Ambos haamini hivyo. Viongozi kama Putin wanasalia madarakani hadi kifo au vinginevyo aondolewe kwa mapinduzi, na serikali mpya ndio inaweza kubeba dhima ya kumfikisha The Hague.

Chanzo: DW