1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahama arejea Ikulu ya Accra

7 Januari 2025

John Dramani Mahama anaapishwa kwa mara ya pili kuwa rais wa Ghana, akikabiliwa na kazi ngumu ya kupambana na ufisadi, ukosefu wa ajira, kupanda kwa gharama za maisha na hali ya kutoridhika miongoni mwa raia.

Ghana  | John Mahama
John Dramani Mahama anayerejea kwenye Ikulu ya Ghana.Picha: Seth/Xinhua/IMAGO

Kiongozi huyo wa upinzani mwenye umri wa miaka 66, alishinda uchaguzi wa tarehe 7 Disemba kwa kiwango kikubwa cha kura, na hivyo kufanikiwa kurejea madarakani kwenye taifa hilo la Afrika Magharibi linaloshikilia nafasi ya pili wa uzalishaji wa kakao.

Soma zaidi: Dramani Mahama ashinda uchaguzi Ghana

Mahama anachukuwa madaraka kutoka kwa Nana Akufo-Addo, ambaye anastaafu baada ya kuhudumu kwa vipindi viwili, na hivyo kuendeleza utamaduni wa kidemokrasia wa Ghana, wa kubadilishana madaraka kwa njia za amani, katika eneo ambalo limetandwa na mapinduzi ya kijeshi na makundi ya uasi.

Kwa mara ya kwanza, Mahama aliingia madarakani mwaka 2012 kufuatia kifo cha Rais John Evans Atta-Mills, na kisha kushinda uchaguzi miezi michache baadaye. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW