1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahasimu katika vita vya Yemen wabadilishana wafungwa

Daniel Gakuba
15 Aprili 2023

Mamia ya wafungwa wa kivita kutoka upande wa Wahouthi na upande wa serikali wamesafirishwa kwa ndege kupelekwa sehemu zinazodhibitiwa na watu wao.

Jemen Sanaa Airport | Gefangenenaustausch
Wafungwa walioachiwa huru wakiwasili kwenye uwanja wa ndege wa SanaaPicha: KHALED ABDULLAH/REUTERS

Kamati ya Kimataifa ya Shirika la Msalaba Mwekundu imearifu leo kuwa mamia ya wafungwa wa kivita, wakiwemo raia wa Saudi Arabia, wameachiwa leo katika makubaliano ya kubadilishana wafungwa baina ya serikali ya Yemen inayoungwa mkono na Saudi Arabia, na kundi la waasi wa Kihouthi wanaoungwa mkono na Iran.

Wafungwa karibu 900 wamesafirishwa kwa ndege kati ya Saudi Arabia na maeneo yanayodhibitiwa na Wahouthi, wakati matumaini ya kumalizika kwa vita vya miaka minane nchini Yemen yakiongezeka.

Ndege ya kwanza  imeondoka katika mji wa Abha wa kusini mwa Saudi Arabia ikibeba wafungwa 120 wa Kihouthi, ikiwa ni kwa mujibu wa afisa wa mahusiano wa Shirika la Msalaba Mwekundu, Jessica Moussan.

Ndege nyingine imeondoka mjini Sanaa, ikiwa na wafungwa 20, 16 miongoni mwao wakiwa raia wa Saudi Arabia, na watatu wakiwa Wasudan.

Chanzo: AFPE 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW