1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mahmoud Abbas ataja kuwa tayari kuiongoza Gaza baada ya vita

18 Januari 2025

Rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas amesema wako tayari kuchukua kikamilifu jukumu la uongozi baada ya vita kumalizika katika Ukanda wa Gaza.

Rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud Abbas
Rais wa mamlaka ya Palestina Mahmoud AbbasPicha: Saudi Press Agency/Newscom/picture alliance

Katika taarifa yake ya kwanza tangu kutangazwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano, Mahmoud Abbas amesema serikali yake imekamilisha maandalizi yote ya kuwajibika kikamilifu huko Gaza, ikiwa ni pamoja na kuandaa mpango wa kuwarejesha waliokimbia makazi yao, kutoa huduma za msingi, usimamizi wa vivuko na ujenzi wa eneo lililoharibiwa na vita.

Kundi la Hamas ambalo limekuwa na udhibiti kamili huko Gaza tangu mwaka 2007 baada ya kushinda uchaguzi wa bunge mwaka 2006, limesema halihitaji kuitawala tena Gaza baada ya mzozo huo.

Soma pia:Mahmoud Abbas: Acheni kuipatia Israel silaha

Mpinzani wake ambaye ni vuguvugu la Fatah, linaongoza serikali inayofahamika kama Mamlaka ya Palestina na kusimamia eneo la Ukingo wa Magharibi linalokaliwa kwa mabavu. Hata hivyo Israel imekuwa ikipinga uongozi wa makundi hayo huko Gaza baada kumalizika kwa mzozo huo.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW