Abbas ahimiza kuondolewa vizingiti vya Israel kuhusu Gaza
14 Februari 2026
Akizungumza kwa niaba ya kiongozi huyo katika mkutano wa kilele wa 39 wa Umoja wa Afrika, Waziri Mkuu wa Palestina Mohammed Mustafa amesema kuondolewa kwa vizingiti hivyo kunahitajika ili kuhakikisha huduma muhimu zinaendelea kutolewa, kuratibu misaada ya kiutu na kuhakikisha waathirika wanapokea matibabu.
Abbas ameituhumu Israel kwa kuendelea kukiuka makubaliano kati yake na wanamgambo wa kipalestina wa Hamas yaliyoanza kutekelezwa mwezi Oktoba mwaka jana na kuungwa mkono na Marekani.
Amesema tangu kutangazwa kwa makubaliano hayo zaidi ya wapalestina 500 wameendelea kuuawa katika Ukanda wa Gaza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Afrika Mahmoud Ali Youssouf, wakati wa ugunzi wa mkutano huo wa siku mbili alisema mauaji ya watu wa Palestina ni lazima yakomeshwe.
Amesema mapigano hayo na mateso kwa watu wa Gaza kunatoa changamoto kubwa katika dhamira ya bara hilo.