Mahojiano na Rais Joseph Kabila wa DRC
17 Oktoba 2007Matangazo
Mwandishi wetu wa Goma, John Kanyunyu, leo alipata nafasi ya kuelekeza maswali kwa Rais Kabila, hasa akianza na nini kitafuata baada ya kumalizika ilani ya wiki tatu kwa muasi Jenerali Laurent Nkunda na wafuasi wake waweke chini silaha, na uhusiano ulivyo baina ya majeshi ya serikali ya Kongo na yale ya Umoja wa Mataifa kwenye uwanja wa mapigano na pia uhusiano baina ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Rwanda.