1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
JangaAsia

Mahujaji 21 wa India wapoteza maisha kwenye ajali ya basi

30 Mei 2024

Mahujaji wa Kihindu wasiopungua 21 wamepoteza maisha leo baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuteleza na kutumbukia kwenye korongo huko sehemu ya jimbo la Kashmir inayodhibitiwa na India.

Ujumbe wa kuwa mwangalifu kwenye moja ya barabara ya milimani India
Ujumbe wa kuwa mwangalifu kwenye moja ya barabara ya milimani IndiaPicha: Onkar Singh Janoti/DW

Afisa wa afya wa eneo hiöp Akhnoor Saleem Khan amesema abiria wengine 35 wamejeruhiwa kwenye ajali hiyo na baadhi yao wapo kwenye hali mahututi. 

Mkasa huo umetokea kwenye mkoa wa Jammu pale basi hilo lililokuwalikikatisha kwenye barabara moja ya milimani kuteleza na kutumbukia kwenye korongo la urefu wa futi 45. 

Soma pia:Mahujaji milioni mbili waanza safari ya Arafa

Mkuu wa sekta ya usafiri wa jimbo mkasa huo ulipotokea Rajinder Shing amesema abiria waliokuwemo kwenye basi hilo ni mahujaji waliokuwa njia kwenye kuzuru hekalu la Wahindu la Shib Khori linalokutikana katika wilaya ya Reasi. 

India ni mojawapo ya nchi zenye kiwango kikubwa cha ajali za barabarani ambazo mara nyingi zinahusitishwa na uendeshaji holela wa vyombo vya moto, ukarabati duni wa miundombinu na magari chakavu.