1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUrusi

Mahusiano ya Urusi,China kuleta utulivu wa kimataifa?

Hawa Bihoga
22 Februari 2023

Urusi na China zimeonesha kuimarisha zaidi mahusiano yao katika mfululizo wa mikutano mjini Moscow, ambayo inatazamwa na mataifa ya Magharibi kama ni ishara ya wazi kwamba Beijing inaweza kutoa msaada mkubwa kwa Kremlin

Russland Moskau | Wladimir Putin und Wang Yi
Picha: Anton Novoderezhkin/ITAR-TASS/IMAGO

Katika mkutano kati ya washirika hao, Rais Vladimir Putin amesema ushirikiano kati ya Beijing na Moscow ni muhimu katika "kuleta utulivu wa hali ya kimataifa".

Mkutano huo unafanyika wakati ambapo China inataka kujenga taswira yake kama mpatanishina inatarajiwa kuelezea kile kilichotajwa kuwa "suluhisho la kisasa" katika mzozo huo wiki hii.

Beijing ambayo imejionesha kutofungamana na upande wowote katika mzozo huo, huku ikidumisha uhusiano wake wa karibu na Kremlin, imemuahakikishia Rais Putin kwamba ipo tayari kuimarisha uhusiano huo wa kina na kimkakati.

Mwanadiplomasia wa ngazi za juu China, Wang Yi, amesema nchi yake ipo tayari kwa ushirikiano zaidi na Urusi bila kujali mabadiliko ya hali ya kimataifa:

Amesema hali ya sasa ya kimataifa ni mbaya na ngumu, lakini uhusiano wa China na Urusi umehimili mtihani wa hali ya kimataifa na kuwa na ukomavu thabiti.

Soma pia:China yaonya kuhusu ongezeko la mzozo wa Ukraine

Ameitaja migogoro na machafuko ya mara kwa mara inayojitokeza, ni fursa kwao.

"Kuna fursa katika machafuko na machafuko yanaweza kugeuzwa kuwa fursa." Alimwambia rais Putin.

Putin:Uhusiano wetu utaleta utulivu wa hali ya kimataifa

Mahusiano kati ya Urusi na nchi za Magharibi upo katika kiwango cha chini kabisa tangu enzi za Vita Baridi huku uhusiano kati ya China na Marekani umekuwa ukikabiliwa na pandashuka chungu mzima.

Rais wa Urusi Vladimir Putin Picha: Sergei Karpukhin/TASS/IMAGO

Akiangazia kuongezeka kwa mvutano wa kimataifa, Rais Putin amemwambia Wang Yi kwamba ushirikiano baina ya Urusi na China ni muhimu kwa kile alichokiita "kuleta utulivu wa hali ya kimataifa":

Soma pia:Rais Vladmir Putin azilaumu nchi za Magharibi kuhusu vita Ukraine

Putin ameyatazama mahusiano ya kimataifa kuwa magumu kwa sasa, tangu kuanguka kwa mfumo wa madola makuu mawili hali imekuwa mbaya zaidi.

"Katika muktadha huu,ushirikiano baina ya China na Urusi ni muhimu kwa utulivu wa hali ya kimataifa."

Putin alimsisititizia Wang kwenye mazungumzo yao yaliohitimishwa kwa urusi kumkaribisha rais wa China Xi Jingpin katika siku za usoni. 

Duma yaidhinisha kusitishwa kwa mkataba wa NEW START

Katika hatua nyingine,baraza la juu la bunge la Urusi limeidhinisha kusitishwa kwa mkataba wa kudhibiti silaha za nyuklia kati ya nchi hiyo na Marekani.

hatua hiyo pia ilifikiwa na baraza la chini la bunge hilo, Duma. Uamuzi huo ulitangazwa na Rais Putin katika hotuba yake ya siku ya Jumanne.

Kusitishwa kwa mkataba huo unaojulikana kama NEW START kumekosolewa vikali na jumuia ya kimataifa, huku Rais Joe Biden wa Marekani akisema Urusi imefanya "kosa kubwa".

Kwenye uwanja wa mapambano,rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amesema vikosi vya Urusi vimeendeleza mashambulizi katika baadhi ya maeneo.

Soma pia:Maoni: Uvamizi wa Urusi Ukraine unamhusu kila raia wa Ulaya

Baadhi ya mikoa ambayo imeshuhudia mfululizo wa mashambulizi ni pamoja na Kherson, Donetsk na Luhansk.

Katika mashambulizi hayo watu kadhaa wameuwawa huku vikosi vya Ukraine vikifanya kila linalowezekana kuzuia mashambulizi ya wanajeshi wa Urusi .

Hata hivyo mwandishi wa zamani wa hotuba za Rais Putin, Abbas Gallyamov, ameiambia DW kwamba, anaamini kiongozi huyo hana mpango mbadala.

Katikauvamizi huo unaokaribia kutimiza mwakaGallyamov amesema, asilimia 100 ya wasomi wa Urusi wanaelewa kuwa hali jumla  ni tete kwenye uwanja wa mapambano.

EU yatangaza vikwazo vipya dhidi ya Urusi vikiwemo vya mafuta

01:26

This browser does not support the video element.