1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mainnoo: Hakuna kuangalia nyuma hadi 'kazi ikamilike'

13 Julai 2024

Tarehe 14 mwezi wa Julai katika uwanja wa Olympia mjini Berlin utachezwa mchezo wa fainali ya michuano ya Euro 2024 kati ya Uhispania na England majira ya saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki

England | Kobbie Mainoo
Kiungo wa kati wa timu ya taifa ya England Kobbie MainoPicha: Odd Andersen/AFP/Getty Images

Kiungo wa kati wa timu ya taifa ya England Kobbie Mainoo amesema  licha ya kuwa na wakati mzuri katika michuano ya Euro 2024 lakini hatofurahia mpaka pale watakapotwaaa ubingwa wa michuano hiyo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 alicheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa mwezi Machi mwaka huu baada ya kuonyesha kiwango kilichowavutia wengi katika klabu yake ya Manchester United na katika mashindano haya ya Euro ameweka rekodi ya kuwa mchezaji mdogo zaidi wa England kuanza mechi ya nusu fainali.

Soma zaidi. UEFA yaridhishwa na kiwango cha maandalizi ya Euro 2024 Ujerumani

Tarehe 14 mwezi wa Julai katika uwanja wa Olympia mjini Berlin utachezwa mchezo wa fainali ya michuano ya Euro 2024 kati ya Uhispania na England majira ya saa nne usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Lamine Yamal wa Uhispania na Jude Belingham wa England wanatarajiwa kuzibeba timu zao katika mchezo huo wa fainali ya michuano hii.