1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MAINZ: Vikosi vya Ujerumani vyatarajiwa kwenda Lebanon

8 Septemba 2006

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani,Frank-Walter Steinmeier anatumai kuwa kikosi cha wanamaji wa Ujerumani,kitapelekwa Lebanon,licha ya matatizo ya hivi sasa.Amesema,anahakika kuwa suluhisho litapatikana kuhusu ujumbe huo.Kwanza lakini,masharti yanayohusika na tume hiyo yapaswa kujadiliwa na Umoja wa Mataifa.Hivyo ndio usafirishaji wa silaha za magendo utaweza kuzuiliwa kwa njia ya maana na kuzuia silaha kuwafikia wanamgambo wa Hezbollah.Waziri Steinmeier alikuwepo Beirut siku ya Alkhamisi ambako alifuatana na washauri 10 wa Kijerumani watakaobakia huko kuwasaidia maafisa wa Ki-Lebanon kulinda usalama katika viwanja vya ndege.Sasa Steinmeier amekwenda Israel.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW