1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Majaji waunga mkono ushindi wa Rais wa Nigeria

27 Februari 2008

ABUJA:

Mahakama maalum nchini Nigeria imeidhinisha ushindi wa Rais Umaru YarÁdua katika uchaguzi uliofanywa Aprili mwaka 2007.Mahakama hiyo imetupilia mbali madai ya wanasiasa wawili wa upinzani kuwa uchaguzi ulifanyiwa udanganyifu mkubwa kwa hivyo ubatilishwe.Lakini majaji watano wameamua kuwa mpinzani mkuu Muhammadu Buhari hakuweza kutoa ushahidi wa kutosha ili kuweza kuchukua hatua hiyo.Majaji hao pia wamekataa madai ya Naibu-Rais wa zamani Atiku Abubakar alietokea wa tatu katika uchaguzi huo ambao waangalizi kutoka Nigeria na nchi za nje wamesema,uligubikwa na udanganyifu.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW