MigogoroAfrika
Kongo, Burundi zashirikiana kuwazuia M23 kuelekea Kusini
1 Februari 2025![Goma, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo](https://static.dw.com/image/71479648_800.webp)
Matangazo
Mapema wiki hii waasi hao wanaoungwa mkono na Rwanda waliuteka mji mkuu wa Kivu Kaskazini wa Goma baada ya mapigano makali na wameapa kusonga mbele hadi kuelekea mji mkuu Kinshasa.
Soma zaidi:Kongo: Mji wa Bukavu wachukua tahadhari dhidi ya M23
Hayo yanajiri muda mfupi baada ya viongozi wa mataifa ya Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), kutoa tamko la dharura la kuiunga mkono Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, katika mapambano yake dhidi ya M23 . SADC ilifanya mkutano wa dharura nchini Zimbabwe kuhusu mzozo unaoendelea mashariki mwa Kongo, ambao umeibua wasiwasi kuhusu usalama wa kikanda.
Kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa, watu 700 wameshauwawa kutokana na mzozo huo katika kipindi kisichozidi wiki moja.