Uganda kufunza wanajeshi wa Equatorial Guinea
16 Februari 2017Matangazo
Msemaji wa jeshi Brigedia Richard Karemire amesema leo kwamba kati ya wanajeshi 100 na 150 wamepelekwa baada ya makubaliano kutiwa saini kati ya nchi hizo mbili mwanzoni mwa mwaka huu. Amesema serikali ya Guinea ya Ikweta ina matumaini kwamba kikosi cha mafunzo na uangalizi kutoka Uganda kitafanya kazi kuelekea kiwango fulani cha utendaji sahihi wa kazi miongoni mwa majeshi ya nchi hiyo. Uganda na Guinea ya Ikweta yenye utajiri mkubwa wa mafuta yanaongozwa na marais wawili walioko madarakani kwa muda mrefu duniani, na wote wanakabiliwa na madai ya kuwa watawala wa kidikteta. Guinea ya Ikweta ndiko rais wa zamani wa Gambia yahya Jammeh alikokimbilia kuishi uhamishoni baada ya kuitawala nchi yake kwa muda wa miaka 22.