1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Majeshi yatumwa katika mpaka wa Mexico na Marekani

26 Oktoba 2018

Wizara ya Ulinzi ya Marekani inapanga kuwatuma wanajeshi mia nane katika mpaka wa Marekani na Mexio kuwakabili wahamiaji ambao msafara wao unaelekea nchini humo.

Mexiko, Chiapas: Flüchtlinge ziehen weiter Richtung Norden
Picha: picture alliance/M. Juarez Lugo

Msemaji wa wizara hiyo amethibitisha kuwa wanajeshi hao wataendelea kutathmini matukio katika mpaka huo. Kulingana na mashirika ya habari nchini Marekani, wanajeshi hao wamepewa majukumu ya kuweka mahema na kujenga uzio. Hata hivyo hawatarijiwi kuwashambulia wahamiaji hao. Kupitia barua pepe msemaji huo wa idara ya ulinzi ya Marekani amesema wamejitolea kuhakikisha desturi nausalama wa mpakani zinalindwa.

Wahamiaji hao waliondoka nchini Honduras tarehe 13 mwezi huu wa Oktoba na kuvuka mpaka wa Guatemala na Mexico wikendi iliyopita. Maafisa wa usalama nchini Mexico wanasema watu 3,630 ndio walio kwenye nsafara huo lakini waandaaji wanasema ni watu 5,500. Idadi hiyo hata hivyo ilipungua baada ya wahamiaji 1,600 kusalia mjini Tapachula, ambapo walikuwa wakisubiri kuwasilisha stakabadhi zao ili watambuliwe kama wakimbizi.

 Tuipoondoka Honduras, lengo letu lilikuwa wazi, kuomba hifadhi nchini Mexico. Lakini sijui kwanini suala hili linazua wasiwasi. Sielewi sababu ya wao kuyatuma majeshi mpakani wakati sisi hatuelekei Marekani. Watu wengi watajaribu kuingia Marekani lakini msafara huu hauelekei huko. Sijui alimweleza Donald Trump kwamba tunakwenda huko. Watu wengi watajaribu kuingia nchini humo lakini kivyao si kupitia msafara huu wa wahamiaji,´´amesema mwaandaaji wa msafara huo Denis Omar Contreras.

Picha: AFP/Getty Images/J. Ordonez

Wahamiaji wengine mia tano pia wanataka kurejea nchini Honduras, wakiwemo 134 ambao walirejeshwa siku ya Jumatano tarehe 24 wiki hii. Rais Donald Trump alisema kwamba sheria za chama cha Democrat zinafanya kuwa vigumu kwao kuwazuia watu mpakani, na kwamba anayatumia majeshi kukabili kile anachokiita dharura ya kitaifa.

Picha: Getty Images/AFP/P. Pardo

Hivi maajuzi Rais wa Marekani alisema kwamba wanajeshi watatumwa katika mpaka huo wa Kusini, na kuwataka wahamiaji hao kurejea katika nchi zao, na kutuma maombi ya kupewa uraia kama mamilioni ya watu wengine wanavyofanya.

Wahamiaji hao hawajakuwa wakifuatilia ripoti na habari zinazowahusu wanapokuwa kwenye msafara wao. Lakini walipoulizwa kuhusu taarifa za Rais Trum anazochapisha kwenye mtandao wake wa Twitter kwamba hatawaruhusu kuingia Marekani, walijibu kwa kusema kuwa Trumpa anafaa kuacha kuwashambulia na kwamba wataendelea kujaribu kuingia nchini Marekani. Kufikia sasa wahamiaji hao wameshasafiri umbali wa takriban maili 95.

Mwandishi: Sophia Chinyezi/APE/DPAE

Mhariri: Mohammed-Abdul Rahman

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW