1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Maji haba nchini Zambia

Miraji Othman28 Julai 2009

Wakati wa Kiangazi maji ni shida nchini zambia

Pampu inayosukuma maji ya kunywa kutoka kisimani nchini ZambiaPicha: DW

Watu bilioni moja duniani kote inawabidi wajikimu bila ya kuwa na maji ya kunywa ya kutosha. Katika nchi ya Zambia ilioko Afrika Mashariki, nusu ya wakaazi hawamudu kupata maji safi ya kunywa, licha ya kwamba nchi hiyo ina rasil mali kubwa ya maji. Mito na maziwa mengi katika nchi hiyo ni nusu ya hifadhi ya maji ya kunywa katika eneo la Kusini mwa Afrika. Hata hivyo, Wa-Zambia wengi inawabidi watembee kwa miguu masafa marefu kuvifikia viini vya maji. Pale maji yanapokuwa hayawezi kunywewa, visima vinaweza kusaidia, lakini navyo vinagharimu fedha nyingi.


Pindi Scolastica Chicha angekuwa na Euro alfu tatu, basi angejuwa nini za kuzifanya. Angechimba kisima ambacho kina pampu ya kusukuma kwa mkono. Angekuwa na kisima hicho, basi bibi huyo, mwenye umri wa miaka 44, angeweza kujiepusha na safari ndefu ya saa tatu kila siku kwenda kwenye mahala pa karib ili kujipatia maji, na badala yake angeshughulikia zaidi shamba lake la mboga. Lakini ilivokuwa ana kipato cha Euro 20 tu kwa mwezi, lililobaki tu ni kuota, na kutambuwa thama kwamba asubuhi ya siku ya pili itambidi aamke mapema akateke maji.

" Mara nyingine naamka saa nane za usiku. Mimi sio peke yangu, kwani huko kwenye maji mara nyingi utakuta mlolongo wa watu unangoja; hivyo sirudi kabla ya saa tatu asubuhi. Huchukuwa ndoo za aina mbali mbali. Kichwani nabeba mtungi wa lita 20, mgongoni debe la lita kumi na katika mikono yote miwili huchukuwa ndoo za lita tano."

Kwa ujumbe, Scolastica Chicha hubeba lita 40, maji ambayo anajuwa wazi kwamba ni tu baada ya kuchemshwa ndipo anapoweza kuyanwa. Mara nyingi hupata tumbo la kuharisha sana yeye na watoto wake. Kuna mtoto wa jirani aliyekufa kutojkana na tumbo la kuendesha. Maji yanayotoka kutoka mashimo yasiohifadhiwa au kutoka mito midogo mara nyingi yanakuwa yamejaa vijidudu na virusi vyenye kusababisha magonjwa. Hayo yamesemwa na Bornface Haangala ambaye anafanya kazi katika tarafa ya Chikuni, kusini mashariki ya Zambia, katika sekta ya mifugo na misitu:

" Maji hapa hupatikana tu katika mwahala fulani, na maji hayo huwa ni machafu na yenye vijidudu. Ni maji yasiofaa kutumika majumbani, na kwa hakika si mazuri kwa unyunyizaji mashambani. Mara nyingi watu inawabidi waende kwa migumu masafa ya kilomita nyingi ili kufikia mahala yalipo maji. Na katika mashimo hayo yaliko maji, sio tu wanakutikana wanadamu lakini pia wanyama- hiyo ina maana wote wawili wanakunywa maji kutoka mahala pamoja.

Nchini Zambia kuna maji ya kutosha na ardhi ilio ya rutuba. Lakini wakati wa kiangazi, baina ya miezi ya Juni na Septemba, viini vingi vya maji vinakauka na kuwa mashimo ya matope. Maji ya kunywa huweza kupatikana tu katika vijiji vya pembezoni, tena kwenye visima.

Kwa kutumia pampu, maji yanaweza kuvutwa kutoka chini, umbali wa mita 40. Hata hivyo, maji safi ya kunywa katika eneo hilo hayawatoshelezi watu wote. Mara fulani wale watu wanaoyahitaji maji sana wanatokea patupu, wagonjwa na walio dhaifu.






Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW