1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Majimbo kadhaa ya Ethiopia yafanya uchaguzi uliocheleweshwa

Daniel Gakuba
30 Septemba 2021

Zaidi ya watu milioni saba katika maeneo matatu ya Ethiopia wanapiga kura katika uchaguzi uliocheleweshwa tangu Juni. Kura katika maeneo ya Somali, ukanda ujulikanao kama Mataifa ya Kusini na Harari ziliahirishwa

Äthiopien Bonga | Wahl
Picha: Shewangizaw Wegayehu/DW

Zaidi ya watu milioni saba katika maeneo matatu ya Ethiopia wanapiga kura katika uchaguzi uliocheleweshwa tangu Juni. Kura katika maeneo ya Somali, ukanda ujulikanao kama Mataifa ya Kusini na Harari ziliahirishwa baada ya ripoti za ukiukaji na ushiriki wa maafisa wa chama kinachotawala katika mchakato huo. Kama ilivyotarajiwa, Chama cha Prosperity cha waziri mkuu Abiy Ahmed kilishinda kwa kura nyingi. Wagombea wachache tu wa upinzani walipata viti bungeni. Katika uchaguzi huo uliochukuliwa kama mtihani wa kwanza wa uchaguzi kwa Waziri mkuu huyo, ni wapinzani wachache tu waliopata viti bungeni. Waziri Mkuu Abiy anatarajiwa kuunda serikali mpya mapema Oktoba. Wakati huo huo, wapiga kura kutoka makabila matano kusini-magharibi mwa Ethiopia watapiga kura ya maoni juu ya kuundwa kwa jimbo la 11 lenye mamlaka ya ndani nchini Ethiopia, na ikiwa watafaulu, litakuwa jimbo jipya la pili lililoundwa tangu Abiy aingie madarakani mwaka 2018. Uchaguzi wa leo Alhamisi, kama ilivyokuwa kwa uchaguzi wa Juni, unafanyika chini ya kiwingu cha vita kaskazini mwa Ethiopia.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW