1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Majimbo zaidi ya 15 ya Marekani yanapiga kura za mchujo

5 Machi 2024

Majimbo zaidi ya 15 ya Marekani yanapiga kura za mchujo leo kuamua wagombea wa urais wa vyama vikuu viwili vya Democratic na Republican kuelekea uchaguzi wa rais wa mwezi Novemba.

Uchaguzi Marekani
Mpiga kura akipiga kura wakati wa upigaji kura wa mapema, siku moja kabla ya uchaguzi wa mchujo wa Super Tuesday, katika kituo cha kupigia kura cha San Francisco City Hall huko San Francisco, California, Machi 4, 2024.Picha: Loren Elliott/REUTERS

Mgombea anayeongoza ndani ya chama cha Republican Donald Trump, anatarajiwa kudhibiti kinyang'anyiro cha uteuzi katika siku muhimu ya kura za mchujo inayojulikana kama Jumanne Kuu. Trump anapambana na mpinzani pekee aliyesalia Nikki Haley ambaye hapewi nafasi kubwa ya kumshinda Trump. Hiyo itakuwa nafasi ya mwisho ya Haley katika kupunguza kasi ya rais huyo wa zamani katika uteuzi wa kuwania urais. Rais wa Marekani Joe Biden hakabiliwi na upinzani mkubwa ndani ya chama chake cha Democratic katika kuteuliwa kuwania muhula wa pili.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW