1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Majina ya Wagombea kutangazwa kesho Liberia

14 Agosti 2005

Monrovia:

Tume ya Uchaguzi nchini Liberia kesho itatangaza majina ya Wagombea 22 wa uchaguzi wa Rais utakaofanywa Oktoba 11 mwaka huu. Uchaguzi una lengo la kufungua ukurasa mpya wa demokrasia baada ya miaka mingi ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Tume imetupilia mbali malalamiko ya vyama vingine kuwa bingwa wa kandanda George Weah asiruhusiwe kugombea kwa sababu amechukua uraia wa Ufaransa wakati alipoichezea timu ya mjini Paris, Saint Germain mwaka 1993 ingawaje watu wengine watano wamepigwa marufuku. Uchaguzi wa Rais na Wabunge unatazamiwa kumaliza kabisa miaka 14 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyosababisha vifo vya watu 250,000 kabla ya Rais wa zamani Charles Taylor kulazimishwa kwenda kuishi uhamishoni Nigeria mwaka 2003 ikiwa ni sehemu ya mapatano ya amani.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW