1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makabiliano kati ya polisi na magenge yaua 9 Brazil

3 Agosti 2023

Watu tisa wameuawa jana katika operesheni ya polisi inayoyalenga magenge ya uhalifu katika mitaa ya mabanda ya mji wa Rio de Janeiro.

Brasilien Polizei
Picha: Buda Mendes/Getty Images

Vifo hivyo ni vya karibuni katika msururu wa misako mikali ya vikosi vya polisi inayofanywa kote nchini Brazil.

Msako huo wa Rio ulifikisha 44 idadi ya vifo kutokana na operesheni ya polisi dhidi ya magenge ya dawa za kulevya nchini Brazil, ikiwemo vifo 14 katika jimbo la Sao Paulo na 19 katika jimbo la kaskazini mashariki la Bahia.

Soma pia: Serikali ya Brazil yadhibiti umiliki wa bunduki

Polisi ya jimbo la Rio imesema maafisa walijibu baada ya kshambuliwa wakati wa kuuvamia mkutano ulioandaliwa na viongozi wa uhalifu katika mitaa ya mabanda ya Complexo da Penha.

Vifo hivyo vinajiri wakati kukiwa na miito ya kufanywa uchunguzi huru wa madai ya ukiukaji unaofanywa na polisi nchini Brazil, ambako vikosi vya usalama vimekabiliwa na tuhuma za ukiukaji wa haki za binaadamu katika vita vyao dhidi ya magenge ya dawa za kulevya yenye silaha nzito.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW