1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaSudan

Makabiliano yapamba moto nchini Sudan

3 Julai 2023

Mapigano makali kati ya vikosi vya majenerali wanaohasimiana yameutikisa mji mkuu wa Sudan, Khartoum jana Jumapili.

Sudan Kämpfe
Picha: Stringer/IMAGESLIVE via ZUMA Press Wire/picture alliance

Wakaazi walioshuhudia mashambulizi hayo wamesema waliamshwa na mapambano ya silaha pamoja na milio ya ndege za kivita.

Hadi sasa, mapambano yaliyoanza katikati ya mwezi Aprili kati ya vikosi vya jeshi rasmi la Sudan chini ya Jenerali  Abdel Fattah al Burhan na wapiganaji wa kikosi cha dharura wa RSF yameshasababisha vifo vya karibu watu 3,000.

Soma zaidi: Mapigano makali kati ya vikosi vya majenerali wanaohasimiana yautikisa mji wa Khartoum nchini Sudan

Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhamiaji - IOM takribani watu milioni 2.2 wamelazimika kuyakimbia makazi yao huku watu karibu watu 645,000 wakikimbilia kuvuka mipaka ya nchi hiyo kulinda usalama wao kutokana na machafuko nchini humo.

Kwa sasa Sudan inakabiliwa pia na magonjwa pamoja na utapia mlo hali inayotishia kuongezeka kwa idadi ya watu wanaoyahama makazi yao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW