1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makabiliano yatokea Lüzerath, Ujerumani

11 Januari 2023

Makabiliano yametokea katika kijiji cha Lüzerath wakati maafisa wa polisi wa Ujerumani walipoingia kuwaondoa wanaharakati wa mazingira.

Proteste in Bremen zu Lützerath
Picha: Richard Wareham/IMAGO

Polisi wanasema mawe na vilipuzi vimevurumishwa kuwalenga maafisa wa usalama waliokuwa wakijaribu kuwaaondoa wanaharakati hao katika kijiji hicho cha magharibi mwa Ujerumani.

Vitu vingine vimerushwa kuwashambulia polisi kutoka kwenye nyumba moja katika eneo la tukio.

Kampuni kubwa ya nishati ya RWE inapanga kuchimba madini ya makaa ya mawe Lüzerath.

Wakaazi walishaondoka na ardhi inamilikiwa na kampuni hiyo, lakini wanaharakati wameyakalia majengo kadhaa kwa miezi sasa na idadi yao imekuwa ikiongezeka katika wiki chache zilizopita.

Polisi wametumia kipaza sauti kuwatangazia wanaharakati waondoke wakati walipoanza operesheni ya kulisafisha eneo hilo leo Jumatano.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW