1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Makadinali kutoka kote duniani wakutana Vatican

26 Juni 2026

Makadinali kutoka sehemu mbalimbali za dunia wamekusanyika mjini Vatican leo kwa mkutano maalumu na wa nadra ulioitishwa na Pope Leo XIV.

Vatican 2026 | Sinodi
Kikao cha Makadinali Vatican mnamo Mei 25, 2026Picha: Yara Nardi/REUTERS

Mkutano huo wa dharura wa makadinali ulianza asubuhi kwa kikao cha kwanza cha kazi, huku majadiliano yakitarajiwa kuendelea hadi kesho Jumamosi.

Kwa mujibu wa Vatican, ajenda za mkutano huo zinajumuisha hali ya dunia kwa ujumla, maendeleo katika teknolojia ya akili mnemba na hatua zinazofuata katika mchakato wa mageuzi ya Sinodi ya Dunia ya Kanisa Katoliki.

Mikutano ya aina hii ni nadra sana. Tofauti na mikutano ya kawaida ya makadinali ambayo inaweza kufanyika mara kadhaa kwa mwaka, mkutano maalumu wa dharura huwakutanisha si tu makadinali wanaoishi Roma, bali makadinali wote zaidi ya 240 kutoka kote duniani.

Mkutano wa makadinali unachukuliwa kuwa chombo muhimu zaidi cha ushauri kwa Papa katika uongozi na maamuzi yanayohusu kanisa Katoliki.

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW