SiasaChina
Makamanda wa China na India wakutana kuondoa mivutano
22 Desemba 2022Matangazo
Mvutano huo ulisababisha mapigano ya umwagaji mkubwa wa damu mnamo mwaka 2020.
Taarifa ya wizara ya ulinzi ya India imesema duru ya 17 ya mazungumzo hayo ilifanyika katika mpaka wa Chushul Moldo upande wa China siku ya Jumanne ingawa haikutowa maelezo yoyote kuhusu ikiwa yamefikiwa makubaliano yoyote ya kumaliza mkwamo uliopo.
Aidha, China nayo pia haijatoa tamko lolote.
Hata hivyo mkutano huo wa makamanda wa kijeshi wa India na China unatarajiwa kupunguza mivutano baada ya kutokea mapigano baina ya wanajeshi wa pande hizo mbili katika jimbo la Arunachal Pradesh upande wa India, chini ya wiki mbili zilizopita.